MAKAMU bingwa wa ligi kuu soka Tanzania bara, Azam fc
wanaanza mawindo ya ligi kuu na kombe la Kagame Juni 15 mwaka huu.
Afisa mtendaji mkuu wa Azam, Saady Kawemba amesema wachezaji
wote wanatakiwa kuripoti kambini siku hiyo isipokuwa wale waliopo timu ya
taifa.
“Tuliwapa wachezaji likizo ya mwezi mmoja, wanarejea kambini
tarehe 15 isipokuwa wale waliopo timu ya taifa, makocha wote watawasili Juni 12
na kuanza maandalizi ya ligi kuu Tanzania bara na kombe la Kagame”. Amesema
Kawemba na kusisitiza: “Kocha mkuu Stewart Hall yupo na anaendelea na kazi
yake, anafanya kazi kuhakikisha mambo yote yanakwenda anavyotaka. Kuhusu
usajili wa wachezaji anamsubiri mwenzake George Nsimbe (kocha msaidizi) ili
wafanye kazi yao”.
0 comments:
Post a Comment