Arturo Vidal akiwasili mazoezini na Ferrari nyekundu
Baada ya kuifanyia Chile kazi inayostahili katika mechi ya Copa America dhidi ya Mexico Jumatatu usiku, kesho yake Jumanne, Arturo Vidal alitua maozeizni akiwa na usafiri unaofaa kwa watu maarufu duniani.
Kiungo huyo wa Juventus alifunga mabao mawili katika sare ya 3-3 na Mexico na siku inayofuata aliwasili mazoezini kwenye uwanja wa Santiago akiwa na gari yake aina ya Ferrari yenye rangi nyekundu.

Vidal alivaa jezi yenye rangi inayofanana na gari yake na rangi hiyo ndio inatumiwa na timu ya taifa ya Chile.
Gari hiyo ya thamani iliwavutiwa wengi na wakabaki kushangaa tu.

0 comments:
Post a Comment