Cheki atavyoonekana msimu ujao.
Petr Cech anajiandaa kuchukua vipimo vya afya katika klabu ya Arsenal baada ya washika bunduki wa London kukamilisha usajili wake kwa dau la paundi milioni 11, ingawa hakuna klabu iliyothibitisha rasmi.
Golikipa huyo mkongwe amemalizana na Arsenal na sasa anakamilisha taratibu kadhaa, kabla ya kutangazwa rasmi.
Kufuatia mazungumzo ya muda mrefu baina ya Chelsea na Arsenal, Cech aliyekuwa tegemeo darajani kwa miaka 10 atasaini mkataba wa miaka mitatu ambao atakuwa analipwa paundi laki moja kwa wiki.
0 comments:
Post a Comment