Mkwaju wa penati wa Carlos Tevez umeipeleka Argentina kwenye hatua ya nusu fainali ikiitupa nje timu ya taifa ya Colombia kwenye mchezo wa robo fainali ya aina yake kuwahi kutokea kwenye historia ya michuano ya Copa America na kuufanya mchezo huo kuvuta hisia za watu wengi tofauti kwenye mashindano yanayoendelea huko nchini Chile.


Tevez aliyeingia dakika ya 73 kuchua nafasi ya Aguero akaibuka shujaa kwa upande wa Argetina kwa kufunga penati yake ikiwa ni penati ya 14 kupigwa kwenye mchezo huo na kuipa Argentina nafasi ya kucheza nusu fainali kwa ushindi wa penati 5-4.


1 Rodriguez – 1-0 Colombia
2 Messi – 1-1
3 Falcao – 2-1 Colombia
4 Garay – 2-2
5 Cuadrado – 3-2 Colombia
6 Banega – 3-3
7 Muriel – 3-3
8 Lavezzi – 3-4 Argentina
9 Cardona – 4-4
10 Biglia – 4-4
11 Zuniga – 4-4
12 Rojo – 4-4
13 Murillo -4-4
14 Tevez – 5-4
Argentina ikatinga nusu fainali kwa ushindi wa penati 5-4 nakuisukumiza nje ya mashindano timu ya Colombia.
0 comments:
Post a Comment