ARGENTINA imeanza kwa sare michuano ya Copa America inayoendelea nchini Chile baada ya usiku wa kuamkia leo kutoka 2-2 dhidi ya Paraguay.
Watu wengi walidhani Argentina ingeibuka na ushindi baada ya Sergio Aguero kufunga goli la kuongoza dakika ya 29', kabla ya Lionel Messi kutumbukiza kitu kambani dakika ya 36'.
Messi amefunga goli hilo kwa mkwaju wa penalti uliotokana na beki wa Paraguay, Miguel Samudio kumuangusha kwenye eneo la hatari Angel di Maria.
Hadi timu zinakwenda mapumziko, Argentina walikuwa wanaongoza 2-0.
Barrios akishangilia goli lake
Kipindi cha pili mambo yalibadilika, Paraguay walifunga goli la kwanza dakika ya 60' kupitia kwa Nelson Valdez na wakasawazisha dakika ya 90' kupitia kwa nyota wa Spartak Moscow, Lucas Barrios.
Valdes
Mechi nyingine ya kundi B imeshuhudiwa Uruguay ikishinda goli 1-0 dhidi ya Jamaica.
Goli pekee la Uruguay limefungwa dakika ya 52' kupitia kwa Cristian Rodriguez.
0 comments:
Post a Comment