MFUNGAJI bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2013/14, Amisi Tambwe, amewachimba mkwara washambuliaji wapya wanaotajwa kusajiliwa na timu kadhaa, akiwamo Mrundi mwenzake anayenukia Simba, Laudit Mavugo, akisema ‘na waletwe tu tuheshimiane’.
Tambwe aliibuka mfungaji bora akipachika mabao 19 wakati huo akiichezea Simba, ambapo licha ya timu hiyo kumaliza katika nafasi ya nne, mwisho wa siku ndiye aliyeibuka shujaa wa kucheka na nyavu.
Hata hivyo, msimu uliomalizika mwezi uliopita, Tambwe alishika nafasi ya pili katika mbio hizo za ufungaji baada ya kufunga mabao 14, nyuma ya kinara Simon Msuva, aliyeibuka kidedea kwa kufunga mabao 17.
Akizungumza na BINGWA kwa mtandao kutoka nchini kwao Burundi, Tambwe alisema atahakikisha anajituma vilivyo msimu ujao ili aweze kupachika mabao mengi iwezekanavyo kutimiza azma yake hiyo.
0 comments:
Post a Comment