Ame Ally (Wa kwanza kulia waliosimama)
MSHAMBULIAJI Amme Ally Amour aliyetamba na kikosi cha Mtibwa Sugar msimu uliopita, ameripotiwa kukamilisha taratibu za kujiunga na makamu bingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) kwa mkataba wa miaka miwili.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba, amekaririwa na mtandao wa Goal.Com akieleza kuwa wamemsajili Amme ili kuiongezea nguvu safu yao ya ushambuliaji ambayo msimu uliopita ilikuwa ikimtegemea zaidi Mrundi Didier Kavumbagu aliyefunga mabao 10 na kuwa kinara wa mabao kwa timu hiyo.
"Tunashukuru kwa kufanikisha dili hili, Amme ni mtu sahihi kwetu ndiyo sababu tunataka kuwa naye. Tunaamini atafanya kazi yake kama alivyokuwa Mtibwa na kutupa taji la Tanzania Bara,” amekaririwa Kawemba.
Amme aliyefunga mabao nane msimu uliopita kabla ya kutua Azam alikuwa akiwaniwa na klabu ya Simba ambayo inahaha kutafuta mshambuliaji atakayeziba pengo la Danny Sserunkuma aliyesitisha mkataba na timu hiyo na kurudi kwao Uganda.
0 comments:
Post a Comment