Tanzania Prisons imemnasa aliyekuwa kocha msaidizi wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', Salum Mayanga na tayari ameanza kukinoa kikosi hicho katika mazoezi yanayoendelea uwanja wa Magereza, Mbeya.
Meneja wa Prisons, Enock Lupyuto ameshindwa kuthibitisha suala hilo akidai yupo njiani kwenda Mbeya kutokea makao makuu Dar es salaam.
Hata hivyo, maamuzi mengi ya Prisons yanafanyika makao makuu ya Magereza, Ukonga, Dar es salaam na ujio wa Enock unaelezwa kuwa ni kuthibitisha jina la Mayanga na kumuandalia mkataba.
Wakati wowote, Prisons itathibitisha kuingia mkataba na Mayanga ambaye usiku wa Juni 20 mwaka huu alitimuliwa kuinoa Stars yeye na bosi wake, Mart Nooij.
0 comments:
Post a Comment