Mchezaji wa zamani wa Simba ambaye alikuwa hapati namba (Kuchoma mahindi), Rahim Juma Abdallah Maarufu kwa jina la Rahim Zenden amesajiliwa na klabu mpya iliyopanda ligi kuu soka Tanzania bara msimu ujao, African Sports ya Tanga.
Rahim, mtoto wa mchezaji na kocha wa zamani wa Simba, Abdallah Kibadeni amemwaga wino kwa Wanakimanumanu akitokea klabu ya Abajalo FC yenye maskazini yake Sinza, kwa Remmy jijini Dar es salaam.
0 comments:
Post a Comment