Alexis Sanchez amekanusha kuzichapa ngumi na mchezaji mwenzake wa Chile, Marcelo Diaz wakiwa kwenye vyumba vya kubadilishia nguo.
Ugomvi uliripotiwa kutokea baina ya wachezaji hao Ijumaa iliyopita ambapo Chile ilishinda 1-0 dhidi ya El Salvador katika mechi ya kirafiki ya kujiandaa na Copa America 2015.
Diaz hakufurahishwa na kitendo cha Sanchez kutaka kupiga mpira wa adhabu ndogo kwenye mechi hiyo wakati yeye ndiye aliyepangwa kupiga mpira yote ya kutenga.
Ripoti nchini Chile zinasema kwamba wawili hao walipigana kwenye vyumba vya kubadilishia nguvu na waliamuriwa na wachezaji wenzao, lakini Sanchez amekanusha taarifa hizo.
"Wote tuko sawa," Sanchez amewaambia waandishi wa habari jana.
"Tulikuwa tunabadilishana mawazo tu, lilikuwa jambo la kawaida, kila kitu tumerekebisha""
0 comments:
Post a Comment