Thursday, June 4, 2015

Gazeti la AS la Hispania limeripoti leo kwamba kiungo gwiji wa Juventus, Andrea Pirlo anatarajia kuachana na soka la ulaya na tayari amekubali ofa ya kujiunga na klabu ya New York City FC inayoshiriki ligi ya Marekani.
Kama tetesi hizo ni kweli, Pirlo mwenye miaka 36 ataungana na mchezaji mwenzake wa zamani wa Chelsea, Frank Lampard na mchezaji wa zamani wa  Barcelona, David Villa.
Kwa mujibu wa As, Pirlo amekubali ofa kutoka New York na fundi huyo wa Italia ataondoka Juve baada ya mechi ya fainali ya ligi ya mabingwa barani ulaya itayopigwa jumamosi mjini Berlin dhidi ya FC Barcelona.
AS wanaeleza zaidi katika stori yao kuwa New York City wamelijadili jina la Pirlo kama walivyofanya kwa Xavi, ingawa kiungo huyo wa Hispania amechagua kwenda klabu ya Al Saad ya Quatar.
Kwa mazingira hayo NYC FC walimuweka Pirlo kama chaguo la pili na tayari ameshaanza mawasiliano na Afisa mtendaji mkuu wa klabu hiyo, Ferran Soriano.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video