Mkurugenzi wa Idara Michezo Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na michezo Leonard Thadeo akipiga mpira kuashiria uzinduzi rasmi wa Airtel Rising Star msimu wa tano. Hafla ya uzinduzi ilifanyika jijini Dar es Salaam 17th June,2015. Mkurugenzi wa Idara Michezo Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na michezo Leonard Thadeo akiwa alama ya uzinduzi wa kampeni ya " Its Now" yenye kuwawezesha vijana kutimiza ndoto zao katika Nyanja mbalimbali kama technologia, michezo na muziki. Wakishuhudia ni Rais wa TFF Jamali Malinzi( kushoto) Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Bi Beatrice Singano Malya (kulia) akifatiwa na mwenyekiti wa soka la vijana Bwana Ayoub Nyenzi Wachezaji wa Airtel Rising Star 2013 ambao sasa wanachezea timu ya wanawake ya Taifa Twiga Stars wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa program ya Airtel Rising Stars ya msimu wa 5 iliyofanyika katika makao makuu ya ofisi za Airtel Tanzania Mkurugenzi wa Idara Michezo Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na michezo Leonard Thadeo (katikati) pamoja na Rais wa TFF Jamali Malinzi( kushoto) Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Bi Beatrice Singano Malya (katikati kulia) akifatiwa na mwenyekiti wa soka la vijana Bwana Ayoub Nyenzi Rais wa TFF Jamali Malinzi akiongea wakati wa uzinduzi wa program ya Airtel Rising Stars msimu wa tano program yenye lengo la kuinua na kusaka vipaji vya soka kwa vijana chini ya miaka 17. Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Bi Beatrice Singano Malya akiongea wakati wa uzinduzi wa program ya Airtel Rising Stars msimu wa tano program yenye lengo la kuinua na kusaka vipaji vya soka kwa vijana chini ya miaka 17.
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania JANA imezindua rasmi msimu wa tano wa mashindano ya soka kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars ambayo yataanza kutimua vumbi Agosti 8 katika ngazi ya awali na kuhitimishwa kwa fainali za Taifa jijini Dar es Salaam kuanzia
Septemba 11 - 21 mwaka huu.
Akiongea na waandishi wa habari kwenye hafla ya uzinduzi jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano amesema kampuni ya Airtel Tanzania ina nia thabiti ya kusaidia maendeleo ya mchezo wa mpira wa miguu hapa nchini na kujivunia mafanikio yaliyotokana na michuano hiyo kwa miaka minne iliyopita.
"Tunaona fahari kwamba michuano ya Airtel Rising Stars imeweza kuibua vipaji vya wachezaji ambao baadhi yao wamechaguliwa kujiunga na timu za taifa za vijana chini ya umri wa miaka 20", alisema Singano.
Kumbukumbu za TFF zinaonyesha kwamba timu ya taifa ya wanawake imeundwa na wachezaji wengi kutoka Airtel Rising Stars ambayo madhumuni yake makubwa ni kuibua na kuendeleza vipaji vya soka kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17.
Singano pia ametangaza kampuni ya Airtel kuingia mkataba na nahodha wa Ivory Coast na kiungo wa Manchester City Yaya Toure katika kampeni mpya iitwayo "It's Now" yenye lengo la kulea na kukuza vipaji barani Afrika kupitia Nyanja mbalimbali kama vile michezo, ikijumuisha mashindano ya Airtel Rising Stars kwa vijana chini ya umri wa miaka 17.
Sehemu nyingine ambazo kampeni hii itazigusa ni mtindo wa maisha na muziki, ambapo wateja watapata ufumbuzi wa masuala mbalimbali ya kiteknolojia ili kuona fursa zinazowazunguka.
Huu ni mwaka wa tano mfululizo kwa michuano ya Airtel Rising Stars kufanyika hapa nchini Tanzania ambayo huanzia ngazi ya chini hadi Taifa. Singano alilipongeza Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania (TFF) pamoja na serikali kupitia Wizara ya Michezo kwa kuiunga mkono kwa dhati michuano ya Airtel Rising Stars tangu ilipoanzishwa nchini mwaka 2011.
Mkurugenzi wa Idara ya michezo katika wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Leonard Thadeo ambaye alikuwa mgeni rasmi, alisema serikali inatambua mchango wa Airtel katika kuibua vipaji vya wanasoka chipukizi.
"Inatuwia vigumu kuwekeza kikamilifu katika bmichezo kwa sababu ya kulemewa na majukumu mengine muhimu ya kijamii ndio maana tunahamasisha sekata binafsi kujitokeza kusaidia na Airtel wanafanya kazi nzuri" alisema Thadeo.
Mwaka huu michuano ya ARS itajumuisha mikoa ya Ilala, Kinondoni,Temeke Mbeya, Mwanza na Morogoro kwa upande wa wavulana na huku upande wa wasichana ukiwakilishwa na mikoa ya Ilala,Kinondoni, Temeke, Mbeya na Arusha.
Kwa upande wake, Rais wa TFF Jamal Malinzi aliipongeza Airtel Tanzania kwa kuwekeza kwenye soka la vijana. "Nawapongeza sana kampuni ya Airtel Tanzania kwa mpango wake huu wa kuwekeza kwenye soka la vijana ambao kwa kweli ndio msingi wa maendeleo wa mpira wa miguu hapa Tanzania na duniani kote", alisema.
Airtel ni kampuni ya simu za mkononi yenye matawi barani Afrika katika nchi za Burkina Fasso, Chad, Congo, Brazzaville, DRC, Gabon, Ghana, Kenye, Madagascar, Malawi, Niger, Nigeria, Rwanda, Selisheli, Sierra-Leone, Tanzania, Uganda na Zambia.
0 comments:
Post a Comment