Aden Rage |
MWENYEKITI wa zamani wa Simba, Ismail Aden Rage amesema
kipigo cha Taifa Stars cha magoli 3-0 walichopata jana dhidi ya Misri kuwania
kufuzu fainali za mataifa ya Afrika (Afcon 2017) kilimfanya apate presha kubwa
na kutaka kuvunja TV ya watu aliyokuwa akitumia kuangalia mechi hiyo mjini
Dodoma.
“Jana nilipata presha kubwa sana, mabao matatu dakika 24 za
mwisho yaliniumiza sana, nililala hofi bin taaban, kidogo nivunje TV ya watu”.
Amesema Rage na kusisitiza: “Kocha (Mart Nooij) atimuliwe, kama Rais wa Malawi
amezuia mshahara wa kocha wa timu ya taifa tena iliyofungwa 2-1 na amesema kama
wanataka kumlipa basi chama cha soka kimlipe, sisi tuliopigwa tatu tunasubiri
nini?, Kocha hana uwezo wowote, taabu
yake hataki ushauri”. Amesema Rage.
Aidha, Rage ambaye ni Mbunge wa Tabora mjini ameponda mfumo wa kucheza mpira wa wazi
waliotumia Stars hususani safu ya ulinzi dhidi ya timu yenye kasi inayomiliki mpira kwa muda mwingi.
“Sio mtaalamu sana wa mpira, lakini nina ‘idea’, unapokwenda
kucheza nje huwezi kuacha mianya mingi kama ile, unatakiwa kucheza Mourinho
Style, unapoona wapinzani ni wazuri, wanamiliki sana mpira, unatakiwa ujilinde
sana na kushambulia kwa kushtukiza”.
“Michezo 18 mnashinda michezo miwili na kufungwa 16,
mnasubiri nini? Taabu yake kocha hasikii ushauri”
0 comments:
Post a Comment