Lallan yupo timu ya taifa ya England inayocheza na Slovenia kesho kuwania kufuzu Euro 2016
Adam Lallana amemshauri Raheem Sterling kuachana na mpango
wa kuihama klabu yake ya Liverpool majira ya kiangazi mwaka huu kwasababu hapendi
kukabiliana naye akiwa na jezi ya timu nyingine msimu ujao.
Lallan amesema Sterling ni mchezaji mkubwa ambaye
anazungumzwa sana na vyombo vya habari, lakini anaamini atabakia Anfield
kwasababu ni mchezaji mwenye kipaji cha juu na rafiki mzuri ambaye atapata
mafanikio zaidi chini ya kocha Brendan
Rodgers.
Sterling amekuwa akihusishwa kuondoka Anfield kutokana na
mazungumzo ya mkataba mpya kukwama, huku Manchester City wakiripotiwa kuvutiwa
na mshambuliaji huyo ambaye amebakiza miaka miwili kwenye mkataba wake.
Awali Manchester City walituma ofa ya paundi milioni 30
wakiitaka saini ya Sterling mwenye umri wa miaka 20, lakini Liverpool wakakataa
dau hilo na sasa Man City wameripotiwa kuongeza dau mpaka paundi milioni 40.
Wakati huo huo Lallana amefurahishwa na kitendo cha
Liverpool kuamua kumbakisha kocha Brendan Roders tofauti na tetesi nyingi
zilizosambaa kwamba anaondoka msimu ujao.
0 comments:
Post a Comment