Na Mwandishi Wetu, Tanga
KUELEKEA Uchaguzi Mkuu wa Klabu ya Coastal Union tayari maandalizi yameanza kukamilika kwa asilimia kubwa ambapo jumla ya wagombea kumi na tano wamejitokeza kuchukua fomu kuwania nafasi mbalimbali za uongozi.
Akizungumza leo ,Ofisa Habari wa Coastal Union,Oscar Assenga amesema katika uchaguzi mkuu nafasi ambazo wagombea wamejitokeza ni Mwenyekitiambapo nafasi hiyo amejitokeza Dokta Ahmed Twaha akiwa hapa mpinzani.
Nafasi ya makamu Mwenyekiti wamejitokeza wagombea wawili ambao ni Salim Amiri na Hussein Abdull Ally ambao watachuana ili kuweza kupatikana mshindi ambayo atachukua nafasi hiyo.
Aidha amesema kuwa katika nafasi ya Kamati ya utendaji wamejitokeza wagombea kumi na mbili ambao watachuana na kubaki wajumbe watano watakaounda kamati ya utendaji.
Amewataja waliojitokeza kuwania nafasi hiyo ni Albert Clement Peter,Omari Mwambasha,Waziri Mohamed,Mohamed Ally “Dondo”,Mohamed Maulid Rajabu,Abubakari Ahmed Machai,Aggrey Ally Mbapu,Hassani Omari Bwana.
Wengine ambao wamejitokeza kuwania nafasi hiyo kuwa ni Abdallah ZuberiAlly “Unenge”,Hassani Ramadhani Muhsin,Albert Clement Peter,Hussein Ally Mwinyi Hamis na Salim Abasi Perembo.
0 comments:
Post a Comment