Cristiano Ronaldo na Lionel Messi wamekuwa wakichuana mara kwa mara kuelekea kuvunja rekodi kubwa zaidi duniani.
Hivi karibu Ronaldo aliifungia Real Madrid goli la 300, Messi akafuatia kwa kuandika rekodi ya kuifungia Barcelona goli la 400.
Haiwezi kupita wiki bila mmojawapo kuvunja baadhi ya rekodi, Ronaldo alifunga goli la 50 msimu huu dhidi ya Malaga mwishoni mwa juma lililopita na mwanasoka bora huyo wa dunia ameweka rekodi ya aina yake.
Kwa kufikisha magoli 50 ndani ya msimu mmoja, Ronaldo sasa amefikisha idadi hiyo ya magoli katika misimu mitano tofauti na kuwa mchezaji wa kwanza kupata mafanikio hayo.
Siku za nyuma Ronaldo alikuwa amefunga magoli 50 katika misimu minne akimpumulia Gwiji wa Brazil, Pele, lakini sasa amekuwa mchezaji wa pekee kama ilivyooneshwa na ukurasa mmoja wa Wikipedia.
Kama mambo yanavyokwenda, msimu ujao anaweza kujikuta anavunja rekodi yake hiyo.
0 comments:
Post a Comment