Sunday, May 31, 2015

Arsene Wenger amesema ana njaa kubwa ya mafanikio baada ya kutwaa kombe la FA na sasa anaelekeza macho yote kwenye taji la ligi kuu England.
Arsenal jana wameitandika Aston Villa 4-0 katika mechi ya fainali ya FA iliyochezwa uwanja wa Wembley na kufanikiwa kutetea ubingwa wao. 
Theo Walcott, Alexis Sanchez, Per Mertesacker na Olivier Giroud walifunga magoli na kuifanya Arsenal iandike rekodi pekee ya kubeba mara 12 kombe la FA.
Mchambuzi wa soka wa Sky Sports, Jamie Carragher anaamini Gunners wanahitaji kuongeza kikosi chao kama wanataka kushindania ubingwa wa Premier League ambao kwa mara ya mwisho walitwaa mwaka 2004.
Kumaliza katika nafasi ya tatu msimu wa 2014/2015 kunawapa Arsenal nafasi ya kuingia moja kwa moja kwenye michuano ya ligi ya mabingwa bara ulaya msimu ujao, lakini Wenger ameamua kuwekeza nguvu zote kwenye kombe la ligi kuu.
"Nadhani tunaweza kupambana," Amesema Mfaransa huyo.
"Kwanini isiwezekane? tulichukua kombe miaka ya nyuma tulipokuwa na nafasi na sasa tunataka  kufanya tena".
"Nina miaka miwili zaidi kwenye mkataba wangu, nitakaa chini na wakurugenzi wangu ili kuona imani yao ikoje". Ameongeza Wenger.
"Njaa yangu ni kubwa mno, lakini nahitaji kufanya vizuri".

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video