Chonongo (kushoto) akiichezea Simba kabla ya kwenda Stand United mwezi desemba mwaka jana.
YANGA wamethibitisha rasmi kuachana na mpango wa kumsajili
Haruna Chanongo baada ya kushindwa kufikia makubaliano.
Katibu mkuu wa Yanga, Dr. Jonas Tiboroa amesema usiku huu
kuwa baada ya kushindwa kumsajili Chanongo sasa wanaendelea kutafuta mchezaji
mwingine.
“Kiukweli dili la chanongo tumeona tuliache kwasababu za
kwetu kama klabu. Tumeshindwa kufikia makubaliano, tumeona tuachane na dili
hili na tutaendelea na mpango mwingine. Tunayo mipango mingi ya kutosha, dili linaposhindikana
tunaweza kupata mchezaji mwingine”. Amesema Tiboroa.
Msimu uliopita Chanongo alikuwa anakipiga kwa mkopo Stand
United akitokea Simba, lakini mkataba huo umekwisha na sasa ni mchezaji huru.
0 comments:
Post a Comment