Mwinyi akisaini mkataba leo
MABINGWA wa ligi kuu soka Tanzania bara, Yanga, leo wamekamilisha usajili wa wachezaji wawili wazawa.
Mlinzi wa kushoto kutokea KMKM ya Zanzibar, Mwinyi Hajji Mngwali amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Yanga, wakati mlinda mlango ambaye hakuwa na nafasi Kagera Sugar, Benedictor Tinocco akisaini mkataba wa miaka mitatu.
Mwinyi alikuwepo kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars kilichofanya vibaya katika michuano ya Cosafa na kutupwa nje hatua ya awali ya makundi.
Hata hivyo mlinzi huyo alicheza mechi moja tu ya mwisho ambayo Taifa Stars walichapwa goli 1-0 na vibonde wenzao Lesotho. Mechi mbili za kwanza, Stars ilichapwa 1-0 na Swaziland na ya pili ikachapwa 2-0 na Madagascar.
Kusajiliwa kwa Mwinyi ni chagamoto kwake kwani anakwenda kuwania nafasi moja na walinzi wengine wa kushoto, Oscar Fanuel Joshua na Edward Charles ambaye mara nyingi anazidiwa kete na Oscar.
Kwa upande wa Tinocco anakwenda kuwania namba na makipa wazoefu, Ally Mustafa 'Bartez' na Deogratius Munishi.
Yanga inaendelea kufanya usajili na sasa wamefikisha wachezaji watatu wa ndani kwani juzi walimsainisha kiungo mshambuliaji kutoka Mbeya City, Deus Kaseke.
0 comments:
Post a Comment