Thursday, May 21, 2015

MATAJIRI wa Azam fc wametaka idadi ya wachezaji wa kigeni ndani ya ligi kuu soka Tanzania bara iongozwe ili waweze kupata Wanandinga wengi wa kiwango juu watakaowawezesha kushindana na timu kubwa barani Afrika pamoja na kuwa chachu kwa vijana wazawa.
Kwa mujibu wa kanuni za ligi kuu Tanzania bara kwasasa, timu zinaruhusiwa kusajili wachache watano (5) wa Kigeni.
Hata hivyo timu za Tanzania zinashindwa kusajili wachezaji wa maana wa kigeni kwasababu hazina wataalamu wa kutafuta vipaji nje ya nchi na Wanasoka wanaokuja nchini wana viwango vinavyofanana au vya chini zaidi kulinganisha na wachezaji wazawa.
Afisa Mtendaji mkuu wa Azam fc, Saad Kawemba amesema klabu hiyo imeshiriki michuano mikubwa barani Afrika kwa miaka mitatu na kujifunza mengi ikiwemo aina ya wachezaji wanaokutana nao kwenye timu za nje.
“Kwa mtazamo wa klabu yetu hasa tukiangalia sasa hivi tunakwenda mwaka wa nne kwenye mashindano ya kimataifa,  kweli kuna haja ya wachezaji wa kigeni kuongezeka ili kutupa nafasi ya kuweza kupigana vizuri”. Amesema Kawemba na kuongeza: “Tunachoomba ni kwamba anayesimamia sheria (TFF) awe makini kuona kuwa wachezaji tunaowaleta kutoka nje wanakuwa na viwango vya juu zaidi ili waweze kuleta changamoto kwa wachezaji wa ndani”.
“Tunakosa nafasi ya wachezaji wa ndani kushindana na wachezaji wa nje wenye uwezo  mzuri, ni tabia ya wachezaji wetu kuridhika mapema, wengi wao wanapopewa nafasi wanashindwa kuzipigania mpaka mwisho.”.
Kawemba amesema kuwa msimu ujao wanatarajia kupandisha vijana wengi kutoka timu ya pili kwenda timu ya kwanza, lakini ingekuwa vizuri zaidi kama wangekutana na wachezaji wengi wa  nje wenye kiwango cha juu.
“Msimu unaokuja tutapandisha vijana takribani saba kutoka timu yetu ya pili kuwaingiza timu ya kwanza, sasa hawa vijana tungependa waweze kufanya mazoezi na wachezaji wenye uwezo mkubwa ili waweze kupata uzoefu wa haraka. Tutakapokuwa na uwezo wa kuwa na mashindano mengi ya kitaifa hapo tunaweza kusema tufunge kuchukua wachezaji  wa nje”. Ameomba Kawemba na kusisitiza: “Tunazungumza hivyo kwasababu tumeweza kupata nafasi ya kushiriki mashindano makubwa kule Lubumbashi DR Congo, tumecheza na Zesco, TP Mazembe na kuona wachezaji wao, pia tumeona kwa wenzetu wa Sudan tuliocheza nao (El Merreikh), ni vizuri kama tunahitaji kushiriki mashindano kwa level ya juu tufungue milango, lakini tuwe na tahadhari kwamba wanaokuja wawe na mchango mkubwa kwenye mpira wetu, wawe ni chachu kwa vijana wetu wazawa ili wafikie kiwango chao

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video