Friday, May 1, 2015

Mrisho Ngassa (kushoto) na Simon Msuva (kulia) wakiwa mazoezini usiku wa jana

MABINGWA wa Tanzania bara, Dar Young Africans wameonesha kuwa hawana masihara kuelekea mechi ya kesho kwani pamoja na safari ndefu ya zaidi ya saa 13, bado wametua Tunisia jana mchana  na kufanya mazoezi.
Wachezaji Yanga walipumzika kidogo tu na baada ya hapo walianza safari ya kwenda mazoezi.

Kikosi cha Yanga kipo mjini Sousse, Tunisia kwa ajili ya kuivaa Etoile du Sahel katika mechi itakayopigwa leo usiku kuanzia majira ya saa 1:00 kwa saa za Tunisia, saa 3:00 usiku kwa hapa Tanzania.

Katika mechi ya kwanza ya Kombe la Shirikishi, iliyopigwa uwanja wa Taifa,Jijini Dar majuma mawili yaliyopita, Yanga na Etoile zilitoka sare ya 1-1.

Pamoja na mashabiki kuonekana wamekata tamaa, kocha wa Yanga amekuwa akisisitiza kwamba watapambana hadi tone la mwisho kutafuta ushindi au sare ya angalau magoli 2-2 ili kusonga mbele moja kwa moja.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video