Thursday, May 21, 2015

Kocha wa Arsenal Arsene Wenger ameonyesha kusikitishwa na vijana wake kwa kukosa makali mbele ya goli katika mchezo dhidi ya Sunderland uliopigwa jana usiku katika uwanja wa Emirates, ambapo timu hizo zilitoka suluhu.
Hii ni mechi ya tatu ambapo Arsenal wameshindwa kupata ushindi katika uwanja wao wa nyumbani, baada ya ile ya Chelsea, Swansea na hii ya Sunderland.
"Tunaweza kusema kuwa tuliutawala mchezo kwa kiasi kikubwa sana lakini kwa sasa tunakosa yale makali na jinsi ya kuzitumia nafasi katika safu yetu ya ushambuliaji,"Wenger aliwaambia waandishi.
"Tulikuwa wachovu kidogo usiku wa jana. Pia hatujafunga ndani ya michezo mitatu tuliyocheza nyumbani na hiyo pengine ni sababu kubwa sana ya sisi kukosa kujiamini.
"Lakini hata hivyo ni lazima utarajie mpinzani wako kucheza vizuri. Tuko katika nafasi nzuri ya kumaliza katika nafasi tatu za juu. Hivyo ngoja tufanikishe hilo.
"Hatukuonekana kama tungepata goli, Kiukweli. Hata kama tulipiga mashuti 20 golini, lakini mara zote kulikuwa kuna kitu kinakosekana. Tulihitaji kitu fulani maalum ili tuweze kupata goli kutokana na ukweli kwaba walilinda kwa umakini wa hali ya juu. Mara zote kulikuwa na kizuizi pale hasa [Sebastian] Coates na [John] O’Shea katika mipira ya krosi.
"Pointi moja tuliyoipata kutoka kwa Man United Jumapili ilikuwa ni muhimu sana. Kama tungeikosa ile tungekuwa na hatari kubwa sanae."

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video