Wednesday, May 20, 2015

KOCHA  Mkuu wa Taifa Stars, Marti Nooij amedai kutorudia makosa yaliyopelekea kupoteza mechi ya kwanza dhidi ya Swaziland kwenye michuano ya kombe la Cosafa.
Akiongelea mchezo wa leo dhidi ya Madagascar, Nooij amesema, makosa yaliyojitokeza katika mchezo dhidi ya Swaziland yamefanyiwa kazi na anaamini vijana wake watafanya vizuri.
Magadascar na Taifa Stars zinashuka dimbani leo jioni majira ya saa 11:00 jioni kwa saa za Afrika kusini, sawa na saa 12:00 jioni kwa saa za Tanzania.
Baadaye usiku majira ya 1:30 kwa saa za Afrika kusini sawa na saa 2:30 kwa saa za Tanzania, Swaziland watachuana na Lesotho.
“Mchezo wa Swaziland tulipata nafasi nzuri za kufunga, lakini washambuliaji wangu hawakuwa makini kuzitumia nafasi hizo, tatizo la kupoteza nafasi nyingi limefanyiwa kazi na nina amini leo vijana watafanya vizuri” alisema Nooij.
Aidha Nooij amesema anataarajia mchezo kuwa mgumu kutokana na Madagascar kuhitaji ushindi wa pili mfululizo, baada ya kuifunga Lesotho katika mchezo wa awali, Nooij ameahidi kufanya vizuri katika mchezo huo.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video