Friday, May 22, 2015

TIMU ya Taifa ya Tanzania,. Taifa Stars leo jioni majira ya saaa 12:00 kwa saa za Afrika mashariki inakamilisha ratiba ya Cosafa kwa kucheza mechi ya mwisho dhidi ya vibonde wenzao wa Lesotho.
Lesotho na Tanzania zote zimepigwa mechi zao mbili zilizopita na kutupwa nje ya michuano hii.
Tanzania ilifungwa 1-0 na Swaziland mechi ya ufunguzi na mechi ya pili ikafa 2-0 mbele ya Madagascar.
Lesotho wao walifungwa 2-1 katika mechi ya kwanza na Madagascar na mechi ya pili wakafungwa 2-0 na Swaziland.
Baada ya mechi hiyo, usiku Stars itapanda ndege kurudi Dar es salaam na jumapili kamati ya utendaji ya TFF itakutana kujadili mwenendo wa timu za taifa hususani Taifa Stars.
Wakati Watanzania wakilia na matokeo pamoja na kiwango bomu cha Taifa Stars,
 jana Namibia imetinga robo fainali ya michuano ya Cosafa baada ya kuisambaratisha Zimbabwe bao 4-1 na sasa watakutana na Zambia katika hatua ya robo fainali.

NAO Mauritius wameifunga Seychelles bao 1-0 lakini haikusaidia kitu, wote wanaenda nyumbani..

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video