Wakala
wa Raheem Sterling, Aidy Ward amedai habari za mshambuliaji huyo kuondoka
Liverpool majira ya kiangazi mwaka huu zimekuzwa kwa kiasi kikubwa na vyombo
vya habari.
Ward
ambaye ni wakala wa muda mrefu wa Sterling amesema yeye pamoja na mchezaji wana
ratiba ya kukutana na maafisa wa Liverpool juma hili na kuanzia hapo wataweka
wazi kila kitu.
Sterling
amebakiza miaka miwili katika mkataba wake wa sasa, lakini amekataa mshahara wa
paundi laki moja kwa juma ulioripotiwa mapema mwaka huu na mazungumzo juu ya
mkataba mpya yakasitishwa mpaka mwishoni mwa msimu huu.
Mwezi uliopita imeelezwa kuwa Sterling hana nia ya kusaini
mkataba mpya na anasubiri ofa za majira ya kiangazi, huku kocha wa
Arsenal, Arsene Wenger akishindwa
kukanusha taarifa za kuitaka saini ya nyota huyo wa Liverpool.
0 comments:
Post a Comment