Tuesday, May 26, 2015


Na Bertha Lumala, Dar es Salaam 
'Huu ni mwaka wa tisa kampuni ya Vodacom Tanzania inadhamini Ligi Kuu Tanzania Bara.'

UONGOZI wa kampuni ya huduma za mawasiliano ya Vodacom Tanzania umesema utaendelea kumwaga fedha kwa ajili ya kuidhamini Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara.

Mkataba wa miaka miwili kati ya kampuni hiyo na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) uliosainiwa mwaka juzi, umemalizika msimu wa 2014/15.

Matina Nkurlu, Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania, ameuambia mtandao huu jijini hapa muda mfupi uliopita kuwa kampuni hiyo itaendelea kuidhamini ligi hiyo na kwamba wako katika mazungumzo na TFF kuhusu suala hilo.

"Nia yetu ni kusaidia sekta ya michezo nchini, hususani mpira wa miguu unaopenbdwa na watu wengi nchini. Tunaendelea na mazungumzo na TFF kuhusu mkataba mpya," amesema Nkurlu.

Kuhusu zawadi za msimu uliopita, meneja huyo amesema tayari wameshakabidhi fedha kwa TFF na wanazungumza na Azam TV ambao watapanga utaratibu mzima wa namna tuzo na zawadi hizo zitakavyotolewac na kuonyeshwa moja kwa moja 'live' kwenye TV.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video