Mashindano
ya Umoja wa Michezo wa shule za Sekondari Tanzania (UMISETA) yameanza leo kwa
mkoa wa Dar es Salaam yakifanyika kwenye viwanja vya nje vya Taifa kwa
ushirikisha shule za wilaya zote za mkoa huo (Kinondoni, Ilala na Temeke) ili
kutafuta timu moja ya Kanda ya Dar es Salaam itakayokwenda kupambana kwenye
michuano ya UMISETA ngazi ya Taifa
itakayofanyika jijini Mwanza kuanzia Juni 8 hadi Juni 21 mwaka huu.
Michuano
hiyo inayoshirikisha michezo yote yaani mpira wa miguu, mpira wa pete, mpira wa
wavu, mpira wa kikapu, riadha, kuruka viunzi, kuruka chini, kurusha kisahani na
mingine mingi ambayo tayari ilianza kusahaulika kwenye sekta ya michezo kwa
upande wa Tanzania.
Mratibu
wa mashindano hayo Abel Mtweve amesema, mashindano hayo ambayo yameanza leo,
yataendelea kesho na keshokutwa yatafikia tamati huku akiongeza kuwa, walimu
wamekuwa wakipata changaoto kubwa katika kuchagua majina ya wanamichezo
watakaounda timu ya Kanda ya Dar es Salaam kutokana na wachezaji wengi kuwa na
vipaji.
“Michuano
hii imeanza leo lakini itaendelea tena kesho na keshokutwa itakuwa mwisho.
Baada ya mashindano tunatarajia kuwa na timu moja kwa michezo yote ambayo
itakwenda Mwanza kwa ajili ya mashindano kama haya lakini kwa ngazi ya Taifa”,
amesema Mwinuka.
“Tumekuwa
na wakati mgumu hasa katika kuchagua majina ya vijana ambao wataunda timu ya
Kanda kutokana na wachezaji wengi kuonesha vipaji vya hali ya juu kwenye kila
mchezo.”, Mwinuka aliongeza.
“Tunatarajia
kuondoka Dar es Salaam Juni 6 kuelekea Mwanza, Juni 7 tutafanya mazoezi kwa
ajili ya kujiweka sawa na michuano hiyo ambapo itaanza rasmi Juni 8 mpaka
itakapomalika Juni 21mwaka huu”, alimaliza Mwinuka.
Serikali
imerejesha michezo shuleni baada ya kuifuta kwa muda mrefu michezo hiyo. Kurudi
kwa michezo hiyo kumetokana na wadau wa michezo kupigia kelele uamuzi wa
serikali kufuta michezo kwenye ngazi ya shule hali iliyopelekea timu za taifa
kuboronga kwenye michuano ya kimataifa.
0 comments:
Post a Comment