Louis van Gaal anaamini msimu ujao Man United itachuana na Chelsea kuwania ubingwa
Louis van Gaal anaamini msimu ujao Manchester United itapambana vikali na mabingwa watarajiwa wa ligi kuu England, Chelsea katika mbio za ubingwa baada ya kukamalisha maandalizi yake ya kabla ya msimu (pre-season) yatayofanyika katika ziara ya Marekani.
Van Gaal alikosoa ziara ya Marekani ambayo tayari ilikuwa imepangwa kabla ya kuanza kazi yake majira ya kiangazi mwaka jana na kwa muda usiozidi wiki mbili aliiongoza klabu kwenda Los Angeles, Washington DC, Detroit, na Miami.
Ingawa United walishinda mechi zote za maandalizi ya msimu, Mholanzi huyo alilaumu ratiba mbaya na waliporudi England Agosti 28 kuanza ligi kuu walivuna pointi 13 tu katika mechi 10 za kwanza.
Miamba ya ligi kuu England itacheza na Club America, San Jose Earthquakes, Barcelona na PSG katika maandalizi ya kabla ya msimu
0 comments:
Post a Comment