Wednesday, May 20, 2015


'Yanga imekuwa mstari wa mbele kwa muda mrefu kupinga udhamini wa Azam TV kwa madai kuwa haulipi.'

WAKATI Simba wanataka walipwe Sh. milioni 400 Azam TV kwa msimu, watani wao wa jadi, Yanga wameikomali kampuni hiyo iwape Shilingi bilioni 1.14 ili mechi zao za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) zionyeshwe moja kwa moja 'live'.

Zacharia Hanspope, mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba na mjumbe wa kamati ya utendaji ya klabu hiyo, alikaririwa jana na moja ya vituo vya redio jijini Dar es Salaam akieleza kuwa Azam TV imekuwa 'ikiwalaza njaa' tangu iliponunua haki za matangazo ya VPL miaka miwili iliyopita.
Alisema Simba imeambulia Sh. milioni 200 katika mechi zote 26 za VPL msimu wa 2014/15, sababu kubwa akidai ni mechi zao kuonyeshwa moja kwa moja na Azam TV.

"Kabla ya mechi zetu kuanza kuonyeshwa na Azam TV, tulikuwa na uhakika wa kuingiza zaidi ya Sh. milioni 600 kwa msimu. Mechi zetu dhidi ya Yanga tulikuwa tunapata zaidi ya Sh. milioni 200 (zote mbili), mechi dhidi ya Azam FC tulikuwa tunaingiza Sh. milioni 50-70," Hanspope alisema na kuongeza.

"Mechi dhidi ya timu nyingine tulikuwa tunapata Sh. milioni 35 na zikishuka sana tulikuwa tunapata Sh. milioni 10. Haikuwahi kutokea Simba kupata chini ya Sh. milioni tatu ya mapato ya mlangoni, lakini msimu huu tulikuwa tunaambulia hadi laki tano."

YANGA WALONGA
Machi 4 mwaka huu, NIPASHE ilitinga katika ofisi za makao makuu ya Yanga zilizopo makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani jijini na kufanya mahojiano na Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Jonas Tiboroha, ambaye alieleza kuwa hawako tayari kuunga mkono udhamini wa Azam TV hadi pale kampuni hiyo itakapotenga fungu la kutosha kwa ajili ya klabu.

"Tumefanya tathmini na kubaini kuwa ili Azam TV waonyeshe moja kwa moja VPL, wanapaswa kutoa Sh. bilioni 16 kwa msimu (Sh. bilioni 1.14 kwa kila klabu - timu zilikuwa 14)," alisema Tiboroha mwenye PhD katika Sayansi ya Michezo.

Hata hivyo, Ligi Kuu ni mali ya TFF na tayari shirikisho hilo lilishaingia ubia wa mitatu na Azam Media wa kuonyesha ligi hiyo ukiwa na thamani ya Sh.5,560,800,000 na ukitarajiwa kumalizika msimu ujao wa 2015/2016.

Azam TV pia wameshanunua haki za matangazo ya ligi nyingine za soka za Afrika Mashariki ikiwamo Ligi Kuu ya Kenya (KPL) na Ligi Kuu ya Uganda.

*Imeandikwa na Sanula Athanas, mwandishi wa michezo mwandamizi wa gazeti la NIPASHE.

CHANZO: IPP MEDIA

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video