Friday, May 1, 2015

HUWEZI kuzungumzia walinzi bora wa pembeni msimu huu wa ligi kuu soka Tanzania bara ukamuacha Hassan Ramadhan Kessy wa Simba.
Kijana huyo mahiri mwenye uwezo kupanda na kushuka, kasi, kupiga krosi na pasi za uhakika zenye ubunifu anasema ‘staili’ ya uchezaji wake ni kipaji binafsi.
Kessy anasema kweye akademi yake (Tanzania Soccer Academy iliyopo Karume, Dar es salaam) alikuwa anacheza winga na alipojiunga na timu ya taifa ya vijana chini ya kocha Marehemu Slyvester Marsh (2009)  akaanza kucheza nafasi ya beki wa kulia na akarudishwa nafasi ya beki wa pembeni kutokana na mfumo wa kocha.
Mlinzi huyu wa pembeni baada ya kupata mafanikio akiwa timu ya Taifa alijiunga na timu B ya Mtibwa Sugar na kutokana na kipaji chake kikubwa, akapandishwa  timu kubwa.
Uwezo mkubwa wa kessy uliwashawishi makocha wengi nchini, lakini mabosi wa Simba hawakufanya makosa katika dirisha dogo la usajili mwezi desemba mwaka jana na kuamua kumsajili.
Kuanzia hapo, Kessy akawaharibia kabisa William Lucian ‘Gallas’ na Masoud Nassor ‘Cholo’ ambao rasmi walianza kukaa benchi muda wote kipindi cha Patrick Phiri na sasa Goran Kopunovic.
Toka asajiliwe Simba amekosa mechi tatu tu, moja dhidi ya Mbeya City ambapo alikuwa na kadi tatu za njano, nyingine mbili ni dhidi ya Kagera Sugar na Mbeya City tena ambazo alijitoa kikosini kutokana na matatizo ya kimaslahi na uongozi wa Simba.
Hata michuano ya Mapinduzi waliyochukua ubingwa januari 13 mwaka huu, Kessy alicheza mechi zote.
Kama hujui Kessy anafanya mazoezi binafsi kwa kiwango kikubwa na anaweza kucheza winga ya kushoto na anatumia miguu yote japokuwa hajawahi kucheza kwa ngazi ya mashindano.
Tumefika sehemu tamu sasa, bila shaka unahitaji kujua mahusiano ya mapenzi ya Kessy, MPENJA BLOG imefanya naye mahojiano maalumu.
Kessy amekiri kuwa na mpenzi kama mwanaume mwingine halisi na kwa taarifa yako jamaa anampenda sana ‘Toto’ wake.
“Mimi nina mpenzi mmoja tu, sichepuki kabisa! Mimi nimejipangia kuwa amaarufu niliopata Simba isiwe sababu ya kuharibu tabia yangu, natumiwa meseji nyingi na wanawake, lakini nachati nao tu”
“Kinachonifanye niwe mtulivu ni siri ya mpira na wazazi, mchango wa wazazi uko poa, wananipa ushauri kabla ya kucheza mechi mpaka ninapokuwa mapumziko, nawashukuru kwa mchango wao.
SIKU SIMBA IKIFUNGWA ANAKAAJE NA MPENZI WAKE?
Kessy anatueleza: “Siku Simba ikipoteza mechi hata muda wa kuwa na mpenzi wangu nakuwa sina, kwasababu nikiwa naye nitakuwa sina furaha, siwezi kuwa naye! Nakuwa najiuliza ile mechi tumepoteza vipi?”
SIKU SIMBA IKISHINDA INAKUWAJE?
“Siku nikishinda mechi nakuwa mtu mwenye furaha, nikifanya vibaya ananikosoa, ananishauri, bwana hapa hujacheza vizuri!, rekebisha kitu fulani na kwa muda mwingi ananipa ushauri na hata watu wakimwambia kitu hawezi kuridhika bila kuniambia”.
JE, MPENZI WA KESSY ANAUJUA MPIRA?
Kessy: “Mpenzi wangu haujui mpira, anaangalia tu uwanjani, lakini ni mshauri mzuri.
ANAWAAMBIA NINI VIJANA WENZAKE KUHUSU MAPENZI?

Kessy anagawa busura: “Nawashauri vijana wenzangu watulie na mpenzi mmoja ambaye ndio kila kitu, anayekuwa na wewe kwenye shida na raha”.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video