Chonongo mweye jezi namba 8 kwenye bukuta yake
Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
'Msimu huu Chanongo alikumbwa na changamoto ya kusimamishwa Simba kwa madai ya utovu wa nidhamu kisha kupigwa faini na kufungiwa mechi tatu na TFF kwa kumpiga teke refa akiwa na timu ya Stand United ya mjini Shinyanga.'
UONGOZI wa Mwadui FC ya Shinyanga umesema umeanza mazungumzo na winga wa zamani wa Simba, Haroun Chanongo, kwa ajili ya kumsajili.
Mbali na Mwadui FC, Chanongo aliyelazimika kutimkia Stand United kwa mkopo baada ya kusimamishwa na uongozi wa Simba kwa muda mfupi baada ya sare ya 1-1 dhidi ya Tanzania Prisons jijini Mbeya Oktoba 25 mwaka jana, pia anawindwa na timu za Toto Africans ya Mwanza na Stand United.
Ramadhani Kilao, Katibu Mkuu wa Mwadui FC, amesema kuwa wamefanya mazungumzo ya awali na mchezaji huyo kuhusu dau la usajili.
"Tumefanya naye mawasiliano, ametueleza kwa sasa ni majeruhi, lakini ametupa muda ili atoe jibu sahihi juu ya kiasi ambacho anahitaji," amesema.
Chanongo amekiri kufanya mazungumzo na Mwadui, na kuweka wazi kwamba Stand United nayo inataka kuendelea naye.
"Mwadui walinipigia na kunieleza juu ya dhamira yao, kwa sasa sitaweza kujibu lolote hadi hapo nitakapofungua 'PoP' (plasta ngumu)," amesema.
Winga huyo alilazimika kufungwa PoP baada ya kuumia katika mechi ambayo Stand ililala 3-2 dhidi ya Yanga jijini Dar es Salaam Aprili 21.
Kuumia huko kumemvurugia mipango yake ya kwenda kufanya majaribio katika klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Katika hatua nyingine, uongozi wa Mwadui FC umesema jana kuwa upo katika hatua za mwisho za kuongeza mkataba na kocha mkuu wao, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’.
Kilao amesema wakimalizana na Julio, wataanza usajili wiki hii, kwa kuwaongezea mikataba nyota waliopandisha timu chini ya Julio.
Julio pia anawania na mabingwa wa Tanzania Bara 1988, Coastal Union, ambao amewanusuru kuporomoka daraja msimu huu.
0 comments:
Post a Comment