Tony Pulis amesema kwamba majibizano kati yake na Arsene Wenger wakati akiwa kocha wa Stoke "yalikuwa ni mazuri mno," linaripoti gazeti la Birmingham Mail.
Na japokuwa hamjui kwa undani Arsene Wenger, Pulis amesema kwamba: "Usikijaji kitabu kwa mauonekano wa kava lake".
Pulis na Wenger mara kadhaa wamekuwa wameonekna wakikwaruzana wakati timu hizo zilipokuwa zikikutana.
Tukio la kukumbukwa kabisa ni pale ambapo Aaron Ramsey alipokanyagwa vibaya na kuvunjwa mguu na mlinzi wa Stoke Ryan Shawcross.
Rafu mbaya: Ryan Shawcross alimvunja mguu Aaron Ramsey mwaka 2010.
Hivyo basi, akielekea katika mchezo katika uwanja wa Emirates hapo kesho, Pulis amesema: “ Ni kweli tulikuwa na hicho kitu wakati niko Stoke. Ilikuwa ni nzuri mno. Nadhani ilikuwa inashangaza kidogo.
“Nilikuwa naadhibiwa vilivyo pale nilipokuwa naenda Emirates na Arsene alikuwa akitaabika pale alipokuja Britania... !
0 comments:
Post a Comment