Mgeni rasmi wa mechi ya Prisons na Mbeya City, Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Abass Kandoro (kushoto) akimkabidhi tuzo James Mwasote.
Mchezaji James Mwasote Ambrose wa timu ya Tanzania Prisons FC leo amekabidhiwa tuzo ya mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa mwezi Machi 2015 kufuatia kuwapiku wachezaji wengine waliokua wakiwania nafasi hiyo.
Tukio hilo limetokea kabla ya kuanza kwa mechi inayoendelea hivi sasa baina ya Prisons na Mbeya City.
Jopo la maalum la makocha ambao hutafuta wachezaji bora kwa kila mchezo na kisha kujumlisha alama za mchezaji kwa kila mchezo na kumpata mchezji bora wa mwezi, ndio hufanya kazi ya kuchagua mchezaji bora kwa kila mwezi.
Hata hivyo imefahamika kuwa Mwasote amepewa tuzo hiyo wakati ni msuguaji benchi mzuri na imebainika kuwa TFF wamejichanganya, kwani tuzo hiyo ilikuwa ni ya James Ambrose wa Polisi Morogoro na sio huyo wa Prisons.
Hivi tunavyozungumza mchezaji huyo bora wa mwezi yuko benchi kwenye mechi muhimu ya Prisons dhidi ya Mbeya City fc na kiukweli hana uhakika wa namba kwenye kikosi cha kwanza.
Hivi tunavyozungumza mchezaji huyo bora wa mwezi yuko benchi kwenye mechi muhimu ya Prisons dhidi ya Mbeya City fc na kiukweli hana uhakika wa namba kwenye kikosi cha kwanza.
0 comments:
Post a Comment