Thursday, May 21, 2015

COSAFA wapo makini kupunguza matumizi! unajua kwanini?
Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars inatarajia kurejea Dar es salaam usiku wa kesho Ijumaa mara baada ya kumaliza mechi yake ya kukamilisha ratiba dhidi ya Lesotho itakayopigwa kesho kuanzia majira ya saa 12:00 jioni kwa saa za Afrika mashariki.
Stars imepoteza mechi mbili za kundi B ambapo ilifungwa 1-0 na Swaziland na jana ikachapwa 2-0 na Madagascar.
Baada ya  kupoteza michezo hiyo miwili,Stars inaungana na Lesotho kutoka kundi B kuaga michuano hiyo, huku kundi A timu za Mauritius na Shelisheli zikiwa zimeshaaga michuano hiyo pia.
Mpaka sasa kundi B la linaongozwa na Madagscar yenye ponti 6 sawa na Swaziland yenye pointi 6 pia zikiwa na tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa, na mchezo wa mwisho utakaowakutanisha kesho ndio utakaoamua nani atatinga hatua ya robo fainali.
Mara baada ya mchezo huo, kocha wa Stars Mart Noij alisema amesikitishwa na matokeo hayo, kwamba hakutegemea kupoteza mchezo dhidi ya Madagascar.

“Timu yangu haikucheza vizuri, haikuweza kutengeneza nafasi nyingi za kufunga , huku wapinzani wetu wakitumia nafasi mbili walizozipata kupata mabao mawili katia mchezo huo” alisema Nooij.
Katika mchezo huo wa jana, Taifa Stars ilishindwa kuonesha makali yake mbele ya timu ya Madagascar na kupelekea kufungwa mabao 2 katika dakika 45 za kipindi cha kwanza.

Sehemu ya ushambuliaji ya Taifa Stars haikuwa na madhara yoyote langoni mwa Madagascar, huku sehemu ya ulinzi ilijikuta ikiwa katika wakati mgumu muda wote kuzuia hatari za washambuliaji wa Madagascar.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video