KUHUSU ishu ile ya kocha mkuu wa Simba aliyemaliza mkataba
wake na kuombwa kuongeza mwingine mambo bado hayajakaa sawa na uongozi wa Simba
umekaa chini kujadili kuhusiana na Kocha huyo ambaye anaonekana kuleta maringo.
Kopunovic ametaka kupewa dola 50,000 (zaidi ya Sh milioni
100) ili asaini mkataba mpya Simba, jambo ambalo uongozi wa klabu hiyo umeona
si sahihi.
SalehJembe
ameripoti kuwa uongozi wa Simba pamoja na viongozi wengine wa kamati ya
utendaji wamekutaka usiku huu kwa ajili ya kujua mustakabali wa kocha huyo.
"Kuna mkutano wa viongozi wamekutana usiku huu, lengo
ni kujua wafanye nini. Inawezekana wakaamua kutafuta kocha mwingine.
"Inaonekana kama Kopunovic anawasumbua na wao wanaona hakuna haja ya
kuendelea kusumbuka naye," kilieleza chanzo.
Kocha huyo raia wa Serbia ameiwezesha Simba kushika nafasi ya tatu, baada ya
hapo ametaka aongezewe mkataba mpya lakini lazima alipwe kiasi hicho kikubwa
cha fedha ambacho kimeonekana ni kikubwa kwa Simba.
Tayari kocha huyo nchini Hungary ambako ndipo yalipo makazi
yake.
0 comments:
Post a Comment