MICHUANO ya COSAFA
inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Mei 17 mpaka Mei 30, 2015 mwaka huu katika
viwanja vya Olympia Park na Moruleng jimbo la North West Province nchini
Afrika Kusini ikishirikisha nchi za Kusini mwa Afrika huku Tanzania na Ghana
zikiwa ni nchi waalikwa.
Kuelekea katika michuano
hiyo, kiungo mshambuliaji wa Simba na Taifa Stars, Ibrahim Ajib ‘Mido’
amemshukuru kocha mkuu wa Simba, Goran Kopunovic kwa kumuamini na kumpa nafasi
iliyosababisha kocha wa Taifa Stars,
Mholanzi, Mart Nooij amjumuishe kwenye kikosi kilichopo Afrika kusini.
‘Kwanza napenda kutanguliza shukurani
kwa mwenyezi Mungu. Pia napenda kutoka shukuruni zangu kwa kocha Goran
(Kopunovic) aliyeniamini na kunipa nafasi mpaka nimefikia hapa nilipo”. Ajib
ameiambia MPENJA BLOG kutokea nchini
Afrika kusini.
Pia nyota huyo kinda amesema
anajipanga kutumia vyema nafasi ya COSAFA kufanya maajabu endapo atapata nafasi
katika kikosi cha kwanza cha Stars.
“Hapa nilipofikia sio mwisho,
nikipata nafasi huku nilipo (Afrika kusini) nitafanya maajabu makubwa kwa uwezo
wa Mungu”. Amesisitiza Ajib.
0 comments:
Post a Comment