Mshambuliaji wa Liverpool Raheem Sterling alizomewa na mashabiki wa klabu hiyo wakati wa utoaji wa tuzo mbalimbali za msimu kwa wachezaji wa timu hiyo.
Sababu kubwa ya kinda huyo raia wa Uingereza kuzomewa ni kutokana na msimamo wake wa kutaka kuondoka klabuni hapo mara baada ya kukataa ofa ya mpya ya mshahara wa paundi 100,000 kwa wiki hali ambayo imewaudhi sana mashabiki wa Liverpool.
Sterling alichaguliwa kuwa mchezaji bora kijana wa msimu huu kwa klabu ya Liverpool.
Raheem Sterling alichaguliwa kuwa mchezaji bora kijana wa msimu huu wa klabu ya Liverpool katika sherehe iliyofanyika huko Echo Arena jana Jumanne.
0 comments:
Post a Comment