TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kesho itacheza
mchezo wake wa kwanza wa kombe la Cosafa dhidi ya Swaziland katika uwanja
wa Royal Bafokeng pembeni kidogo ya jiji la Rustenburg kuanzia majira ya saa
1:30 jioni kwa saa za Afrika Kusini na saa 2:30 kwa saa za Afrika mashariki.
Kuelekea katika mechi hiyo kocha msaidizi wa zamani wa Taifa
Stars na sasa kocha mkuu wa Coastal Union, Jamhuri Kiwhelo ‘Julio’
amefurahishwa na uteuzi wa baadhi ya wachezaji vijana, lakini amesema wangekuwa
wengi zaidi kuliko wakongwe ili kujenga timu ya baadaye.
“Kilichonifurahisha ni uteuzi wa baadhi ya wachezaji wadogo
kama Ajib (Ibrahim), Ndemla (Said), wachezaji kama hawa wangekuwa wengi katika
kipindi hiki cha mashindano, hakika ingetusaidia kutuweka vizuri katika
mashindano yajayo”. Amesema Julio na kusisitiza: “Ukiangalia
timu za wenzetu utakuta kuna vijana wengi kwenye timu kuliko wakongwe, kwa
mfano nchi kama Ivory Coast, ilikuja hapa (Tanzania) na timu ya vijana kama
vile Kipre Tchetche na Michael Balou wa Azam fc, leo hii wanatusumbua katika
ligi ya nyumbani, kwahiyo tungechukua wachezaji wengi wadogo kuliko wakongwe
kama Aggrey Morris, vijana wakipata uzoefu katika mashindano kama hayo wanaweza
kutengeneza mpira wao. Wachezaji wakongwe wangetolewa".
Kuhusu mechi ya kesho, Julio amesema: "Mechi ya kesho mwalimu amesema maandalizi ni mazuri, kama ni mazuri kweli basi tusubiri, naamini wachezaji watafanya kazi yao, kwasababu walifanya mazoezi vizuri, walipata uwanja mzuri"
Kuhusu mechi ya kesho, Julio amesema: "Mechi ya kesho mwalimu amesema maandalizi ni mazuri, kama ni mazuri kweli basi tusubiri, naamini wachezaji watafanya kazi yao, kwasababu walifanya mazoezi vizuri, walipata uwanja mzuri"
0 comments:
Post a Comment