Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
'Kaseja amewahi kuzidakia klabu kongwe nchini, Simba na Yanga huku akituhumiwa kuzihujumu.'
KLABU ya Stand United imetenga dau la Tsh. milioni 40 kwa ajili ya kumnyakua kipa mkongwe nchini Juma Kaseja ambaye alijiondoa kwenye kikosi cha Yanga msimu uliopita kutokana na kuwekwa benchi.
Mkurugenzi wa ufundi wa Stand United, Muhibu Kanu, amesema kuwa wanataka kukiboresha kikosi chao kwa kusajili wachezaji wenye majina makubwa ili waweze kufanya vizuri msimu ujao.
“Tuna fungu kubwa la usajili ambalo tumepewa na wafadhili wetu, fungu ambalo linatupa ruhusa ya kusajili mchezaji yeyote tunayemtaka kutoka Simba, Yanga na hata Azam. Lengo letu ni kuifanya Stand kuwa timu bora na kuchukua ubingwa msimu ujao,”amesema Kanu.
Kwa sasa Kaseja ni mchezaji huru baada ya kujiondoa Yanga na klabu hiyo ilimfungulia mashtaka ikimdai mamilioni ya shilingi kwa madai ya kukatisha mkataba.
0 comments:
Post a Comment