Sunday, May 17, 2015

MANCHESTER United wanatarajia kuipa Arsenal kipigo cha pili msimu huu wanapokutana leo katika mechi ya ligi kuu England  uwanja wa Old Trafford.
Louis van Gaal alishinda 2-1dhidi ya Arsenal katika uwanja wa Emirates mwezi novemba mwaka jana na leo anahitaji kushinda kwa mara ya pili msimu huu.
Baada ya kupoteza mechi tatu mfululizo, United walishinda dhidi ya Crystal Palace wiki iliyopita na kimahesabu wanahitaji pointi moja tu kufuzu ligi ya mabingwa Ulaya msimu ujao, ingawa Liverpool wanaoshika nafasi ya tano wapo nyuma kwa pointi sita, wana wastani mbaya wa magoli ya kufunga na kufungwa.
Gunners ambao walishinda 2-1 dhidi ya Man United Old Trafford katika mechi ya raundi ya sita ya kombe la FA, leo wanahitaji kushinda ili kuipiku Man City kushika nafasi ya pili msimu huu.

HABARI ZA TIMU

Wayne Rooney na Luke Shaw wanaikosa mechi ya leo kutokana na majeruhi waliyopata wiki iliyopita kwenye mechi dhidi ya Crystal Palace.
Marcos Rojo, Angel Di Maria na Robin van Persie wako hatarini kuikosa mechi hii wakati Michael Carrick na Rafael wako nje kwa mechi zote za ligi kuu zilizosalia.
Danny Welbeck anakosa nafasi ya kucheza dhidi ya timu yake ya zamani kwasababu ya majeruhi ya goti na Mathieu Debuchy hayupo pia.

TAKWIMU MUHIMU

Manchester United hawajawahi kufungwa katika mechi 7 za nyumbani dhidi ya Arsenal (Wameshinda 6, sare 1) tangu walipofungwa 1-0 mwezi septemba 2006.
Wayne Rooney amefunga magoli 11 dhidi ya Arsenal katika mechi za ligi kuu England, lakini amefunga magoli mengi zaidi dhidi ya Aston Villa (13) na Newcastel (12).
United hawajaruhusu kufungwa zaidi ya goli moja katika uwanja wa nyumbani dhidi ya Arsenal na kupoteza mechi ya ligi tangu februari 1979.
Arsenal inaweza kuwa timu ya nne kihistoria kuifunga Man United mara mbili Old Trafford katika msimu huo huo. Timu nyingine zilizowahi kufanya hivi ni Chelsea (2004/2005), Tottenham (1989/90) na Aston Villa (1919/20).
Manchester United wameshindwa kuzuia kufungwa goli katika mechi saba walizocheza na mara ya mwisho kucheza mechi 8 bila kuruhusu nyavu zao kuguswa ilikuwa septemba 2001.
Arsenal wameshinda mechi tano zilizopita za ugenini, huu ni mwenendo mzuri zaidi kuwahi kutokea tangu walipofanya hivyo septemba 2013 (walishinda mechi 8).


0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video