Singano (wapi kushoto)
TIMU ya Simba imeshindwa jaribio lake la kuinasa tena saini
ya kiungo mshambuliaji wakeo, Ramadhani Singano ‘Messi’ baada ya kutaja dau wanalodia
ni kubwa la shilingi milioni 50.
Katika ripoti iliyoandikwa na Salehjembe leo, inafafanua
kuwa mkataba wa Singano umemalizika hivi karibuni mara baada ya kumalizika kwa
msimu wa 2014/15 na inavyoonekana hali ni ngumu kwa kuwa klabu hiyo imeshindwa
kumshawishi kusaini mkataba mpya.
Chanzo cha habari kutoka ndani ya uongozi wa timu hiyo
kimesema kuwa Singano amegoma kusaini kwa dau la shilingi milioni 30 mkataba wa
miaka miwili.
“Dili la Messi la kusaini mkataba mwingine wa kuichezea
Simba limeshindikana, baada ya pande zote mbili kwa maana ya mchezaji na
viongozi kushindwa kufikia muafaka.
“Alitaka milioni 50, viongozi walitaka kumpa milioni 30,
sawa na dau la (Said) Ndemla, yeye akalikataa. Yote hayo yanatokana na usajili
wa Mkude (Jonas) ambaye alipewa shilingi milioni 60 na gari la kutembelea
Toyota Mark 11 Grande, hivyo wachezaji wengine nao wanataka kiasi kikubwa cha
fedha wakiamini watapata,” kilisema chanzo hicho.
0 comments:
Post a Comment