Sunday, May 31, 2015

Kiongera

SIKU moja baada ya Yanga kutangaza kufunga usajili wa wachezaji wa ndani, watani wao wa jadi, Simba nao wametangaza kufunga usajili huo wa wanandinga wazawa.
Simba tayari imeshasajili wachezaji watano wazawa ambao ni Mohamed Fakhi (JKT Ruvu), Samih Hajji Nuhu (Azam fc), Peter Mwalyanzi (Mbeya City), Musa Mgosi (Mtibwa Sugar) na mlinda mlango Mohammed Abrahim (JKU).
Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesema sasa wanatupia macho kimataifa na wana mpango wa kumrejesha mshambuliaji wao wa zamani, Mkenya, Paul Kiongera.


“Sisi tumekamilisha usajili wa wachezaji wa ndani, sasa tunaangalia kimataifa. Kuna baadhi ya wachezaji wa kimataifa tumezungumza nao, jana tulikuwa tunamuangalia Kiongera (Paul), tumeona bado yuko bomba, tunafikiria ni wakati muafaka wa kumrejesha”. Amesema Hans Poppe na kusisitiza: “Hatujafikia maamuzi ya kumrudisha kiongera, lakini wengi wetu tunakubaliana kuwa yuko sawasawa".

Kiongera kwa sasa anaitumkia KCB kwa mkopo akitokea Simba baada ya kupona majeraha yake ya goti.

"Kiongera ni mchezaji wetu, tumejiridhisha kwamba amepona vizuri maana sasa anacheza zaidi ya dakika 70. Tunamrudisha hapa Tanzania kwa ajili ya kikosi chetu cha msimu ujao," amesema Hanspope.

Kiongera aliumia goti la mguu wa kulia katika mechi yao ya kwanza ya Ligi Kuu Bara msimu uliopita dhidi ya Coastal Union kwenye Uwanja wa Taifa Septemba 21, 2014 na kumlazimu kukaa nje ya uwanja kwa miezi mingi.

Wakati Simba wakitangaza leo kumaliza usajili wa ndani, Yanga walifanya hivyo jana muda mfupi baada ya kuinasa saini ya Malimi Busungu kutoka Mgambo JKT.
Yanga wameshasajili wachezaji wanne wa ndani ambao ni Deus Kaseke (Mbeya City), Mwinyi Hajji (KMKM), Benedictor Tinocco (Kagera Sugar) na Malimi Busungu (Mgambo JKT).

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video