SIMBA inaendelea na usajili wa kimataifa lakini imepanga
kuzunguka na kufanya utafiti kwa nchi tano hapa Afrika huku lengo likiwa ni
kumtafuta straika mmoja tu atakayekuja kuziba pengo la Mganda, Dan Sserunkuma.
Simba imepanga kufanya usajili huo kwa kuwa
tayari inaye straika mwingine atakayejiunga na timu hiyo msimu ujao, Mkenya,
Paul Kiongera, anayetokea KCB ya Kenya alikokuwa akicheza kwa mkopo na
kuimarisha kiwango chake baada ya kukaa nje kwa muda mrefu akiuguza majeraha
aliyokuwa nayo baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans
Poppe, amesema nchi walizopanga kwenda kuangalia mchezaji wa nafasi hiyo ni
pamoja na Burundi, Kenya, Senegal, Ghana na Uganda.
“Tunaamini tunaweza kupata straika mzuri mwenye uwezo wa juu
katika nchi tano ambazo tuna imani nazo katika nafasi hiyo, tunaangalia katika
nchi za Burundi, Kenya, Senegal, Ghana na Uganda.
"Lengo ni straika mmoja, tukimaliza hapo tutakuwa na
wachezaji wageni wanne na hiyo nafasi moja tutaangalia kama kutakuwa na usajili
wa nafasi yoyote ya lazima,” alisema Hans Poppe.
Simba imeamua kuachana na Waganda wawili, Simon Sserunkuma
na Dan Sserunkuma na sasa imebaki na Emmanuel Okwi, Juuko Murshid na Mkenya,
Kiongera anayerejea.
0 comments:
Post a Comment