Wednesday, May 20, 2015

Idd Salim


Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
'Salim ndiye aliyekuwa kocha wa makipa wa Gor Mahia wakati Ivo Mapunda akiidakia klabu hiyo 2013.'

MABINGWA mara 18 wa Tanzania Bara,  Simba wametinga nchini Kenya kusaka saini ya kocha wa makipa wa AFC Leopards, Iddi Salim ili kujiweka sawa kabla ya kuanza kwa msimu wa 2015/16 wa Ligi Kuu ya Bara.

Kwa mujibu wa Said Tully, mjumbe wa kamati ya utendaji ya Simba, kocha huyo wa zamani wa mabingwa wa Kenya, Gor Mahia, ambaye alijiunga na AFC Leopards mapema mwaka huu, anakamata nafasi ya kwanza katika orodha ya makocha wanaowaniwa na Wekundu wa Msimbazi kwa sasa, orodha ambayo pia ina jina la kocha wa makipa wa zamani wa Yanga na Coastal Union, Mkenya Razak Siwa.

Tully amekaririwa na moja ya mitandao ya michezo ya Kenya leo akieleza kuwa wanahitaji kukutana na Salim kuzungumzia maslahi yake kabla ya kufanya uamuzi.

"Ni kweli, tunamhitaji na tayari tumeshaanza kumfuatilia, lakini kwanza kabisa kabla ya yote tunahitaji kuzungumza naye kuona kama tunaweza kutimiza mahitaji yake binafsi ikiwa ni pamoja na mshahara na maslahi mengine.

"Tumeona pia makocha wengine kutoka Kenya ambao wametuvutia katika kazi hiyo. Miongoni mwao ni Razak Siwa ambaye alikuwa  Yanga," amesema Tully.

Ikiwa dili hilo likifanikiwa, Salim atafanya kazi kwa mara nyingine na kipa wa kimataifa, Ivo Mapunda, ambaye alimfundisha wakiwa Gor Mahia 2013.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video