Hans Poppe |
BAADA ya kumnasa kiungo mshambuliaji wa Mbeya City, Peter
Mwalyanzi na kumsainisha mkataba wa miaka miwili leo, uongozi wa Simba umesema
kesho utatangaza kumsajili nyota mwingine ambaye hajatajwa jina lake.
Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba, Zacharia Hans
Poppe amesema kocha alipendekeza apatikane kiungo mshambuliaji ambaye wamempata
Mwalyanzi, lakini hawakumuhitaji Deus Kaseke kama alivyokuwa inaripotiwa na
vyombo vya habari.
Kuhusu kocha mkuu atakayerithi mikoba ya kocha Goran
Kopunovic, Hans Poppe amesema kufikia jumatano ya wiki ijayo watakuwa wamempata
na kutangaza jina lake.
“Tumeshajadili majina ya makocha sita na tumeongeza mwingine
mmoja. Kila mmoja tunamjadili na kumpa pointi, nadhani kufikia jumatano panapo
majaaliwa tutakuwa tumepata jina la kocha”. Amesema Hans Poppe.
0 comments:
Post a Comment