Imeripotiwa kuwa Rais
wa FIFA, Sepp Blatter anaogopa kuingia Marekani kutokana na uchunguzi wa FBI
unaoendelea hivi sasa kuhusu uongozi wa FIFA kuzizawadia nchi za Russia na
Qatar kuandaa Kombe la Dunia 2018 na 2022.
Kupitia kipindi cha
masuala ya uchunguzi cha ESPN
kiitwacho E:60, Jumanne hii, kilimwangalia Blatter. Kama walivyoripoti
kupitia akaunti yao ya mtandao wa Twitter, inaonekana Blatter, 79, hataki
kuingia Marekani kwa sababu ya uchunguzi juu ya rushwa na ufisadi endapo kama
vilitumika katika kuzawadia nchi husika kuandaa Kombe la Dunia.
Lakini, kama
ilivyoripotiwa na Bryan Swanson wa Sky
Sports, FIFA ilijibu haraka tuhuma hizi. Kupitia akaunti ya Bryan Swanson
ya twitter, @skysports_bryan, twiti hiyo ilisema hivi, [FIFA: ‘Si kweli kabisa’
kudai kuwa Sepp Blatter kakataa kwenda Marekani ‘kwa sababu ya maombi ya FBI’]
Hapo kabla, FIFA
haikuona ushahidi wowote juu ya rushwa au makosa yoyote katika uchunguzi wake. Lakini FBI
iliamua kuendelea na uchunguzi wake, ambao una miaka mitatu sasa.
Inategemewa FBI itaomba
kuona ripoti fupi ya Michael Garcia iliyotolewa kupitia BBC
Sport kwa kuwa yeye ndiye aliyeendesha uchunguzi mzima wa FIFA.
Lakini pia kupitia
Charles Sale wa gazeti la Uingereza, Daily
Mail aliripoti, “UEFA imezidi kuwashuku wanasheria wa FIFA kuwa
watabadilisha ripoti ya Michael Garcia ili kumlinda Rais Sepp Blatter” wakati
ripoti mpya itakapotolewa hapo baadaye.
Sale anaamini Blatter
kaingia Marekani mara moja tu tangu kura ya kuandaa Kombe la Dunia ilipopigwa
mwaka 2010. Anasema, “Blatter hataki kuulizwa maswali” juu ya mambo ya ufisadi na
rushwa. Sale pia alithibitisha kuwa Chuck Blazer, mwanachama wa zamani wa FIFA,
anatumiwa kama mtoa habari kwa kazi hiyo ya FBI.
Hapo kabla, kipindi cha
ESPN kilirushwa hewani mahsusi kwa
ajili ya mazingira yasiyo ya kibinadamu kwa wale wanaofanya kazi kwenye viwanja
na miundombinu itakayotumika kwa ajili ya Kombe la Dunia, mwaka 2022.
Blatter amebaki kuwa
Rais wa FIFA kwa miaka 17 na bado amepanga kugombania kwa mara yake ya mwisho
katika uchaguzi wa mwaka huu.
Anategemewa kugombania
kiti hicho na Prince Ali bin al-Hussein wa Jordan, Michael van Praag wa
Uholanzi na mchezaji wa zamani wa Ureno, Luis Figo. Kama kituo cha habari, BBC kilivyoripoti, wapinzani hao wote
watatu walitegemewa kuja na “mbinu moja”, ambayo ingelenga kumfanikisha mgombea
mmoja kati yao ili tu kumwangusha
Blatter, lakini hilo limeshindikana.
Owen Gibson wa gazeti
la Uingereza, Guardian aliripoti
“Blatter anabaki kuwa mgombea mwenye nguvu” na atashinda kwa mara nyingine
tena.
0 comments:
Post a Comment