Arsene Wenger amesema kuwa anatarajia Alexis Sanchez atakuwepo katika mchezo wa fainali ya kombe la FA dhidi ya Aston Villa, lakini ana hofu kubwa ya mchezaji huyo kukosa michezo ya mwanzoni mwa msimu wa ligi kuu msimu ujao.
Wenger amesema hayo kutokana na ukweli kwamba Sanchez anatarajia kutumia muda mwingi na timu yake ya taifa katika michuano ya Copa America, ambayo Chile ndio watakuwa wenyeji wa michuano hiyo.
Katika mchezo wa fainali dhidi ya Aston Villa utakaopigwa mei 30, Sanchez atakuwepo, lakini hali itakuwa ndivyo sivyo endapo Chile itafika mbali zaidi katika michuano ya Copa America ambayo kilele chake ni Julai 4, itasababisha mchezaji huyo kuchoka sana hivyo kupumzika mwanzoni mwa msimu.
"Kama wakifika mbali sana, atakosa mechi za ligi mwanzoni mwa msimu," Wenger alisema.
Sanchez, 26, amefunga mabao 19 katika michuano yote tangu aliposajiliwa kutoka Barcelona kwa ada ya Paundi milioni 32, punde tu baada ya michuano ya kombe la dunia kuisha.
Michuano ya Copa America itaanza juni 11 wakati ligi kuu nchini Uingereza msimu wa 2015-16 itaanza Agosti 8.

0 comments:
Post a Comment