Friday, May 1, 2015


Na Richard Bakana, Dar es Salaam.
Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara ikiwa inaelekea Ukingoni na Bingwa akijulikana kuwa ni Dar  Young Africans ikipokea kijiti kutoka kwa Azam FC baada ya kunyakua taji hilo mwaka jana, Mfungaji bora kwa sasa wa Azam FC, Didier Kavumbagu amempatia mkono wa kwaheri Simon Msuva wa Yanga katika kuwania Kiatu cha Ufumania Nyavu wa VPL huku akidai kuwa majeruhi katika kikosi chao na yeye kutocheza mchezo mmoja ndio sababu ya kuachwa mbali.
Akiongea  leo muda mfupi baada ya kutoka mazoezini, Kavumbagu amesema kuwa yeye hawanii tena tuzo hiyo ya mfungaji bora kufuatia mwanya mkubwa ambao ameachwa na Msuva, licha ya Nyota huyo wa zamani wa Yanga kuongoza safu ya ufumania nyavu wa ligi hiyo kwa muda mrefu zaidi na sasa anaelekezea nguvu zake katika mchezo dhidi ya Simba utakaopigwa siku ya Jumapili wiki hii katika Uwanja wa Taifa.
“Unajua sisi tulipata majeruhi zaidi ya sita kikosini, pia sikucheza mchezo mmoja, nilikuwa na kadi tatu za njano , kwa sasa siwanii ufungaji bora, kikubwa ninajipanga zaidi” Amesema Kavumbagu Ambaye pia ni mshambuliaji wa kutumainiwa wa kikosi cha timu ya Taifa ya Burundi.
Nyota huyo ambaye mwaka jana alikuwa mfungaji bora wa klabu ya Yanga hadi sasa ana jumla ya mabao 10  Rashid Mandawa wa Kagera Sugar, huku Simon Msuva akiongoza usukani akifumania nyavu mara 17 akifuatiwa na Amissi Tambwe pia wa Yanga mwenye magoli 14.NgassanaMsuva1
Didier amejitofautisha na Msuva kwa kusema kuwa yeye katika mabao yote aliyofunga akiwa Azam hakuna bao hata moja la penati tofauti na Msuva ambaye amepewa penati nyingi kitu ambacho kimemfanya azidi kuwa juu.
“Inatakiwa uangalie wewe mwenyewe, Yanga wamepewa penati ngapi ambazo Msuva anafunga hata kama wamejiangusha, lakini sisi hakuna penati hata moja ambayo tumepewa kwani sisi hatufanyiwi faulo?” Amesema Kavumbagu huku akiuliza swali.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video