GOLI pekee la Ally Bilal ‘Benzema’ mapema dakika
ya 12’ kipindi cha kwanza limewapa JKT Ruvu pointi tatu muhimu dhidi ya Mgambo
JKT katika mechi ya ligi kuu soka Tanzania bara iliyomalizika jioni hii uwanja
wa CCM Mkwakwani, Tanga.
Kikosi hicho cha Fred Minziro kimefikisha pointi
31 baada ya kushuka dimbani mara 25 na sasa kimebakisha mechi moja dhidi ya
Simba.
Kwa mazingira hayo JKT Ruvu ambao wamepanda kutoka
nafasi ya 8 mpaka ya sita wamejikwamua kutoka mstari mwekundu wa kushuka
daraja.
Mgambo JKT wameendelea kuwa na pointi zao 28 baada
ya kucheza mechi 25 na sasa wamebakiwa na mechi moja dhidi ya Azam fc
itayopigwa mei 9 mwaka huu uwanja wa Azam Complex, Dar es salaam.
0 comments:
Post a Comment