RASMI: Kituo cha Televisheni cha Azam TV kimepata haki ya kurusha moja kwa moja 'Live' mpambano wa kombe la shirikisho hatua ya 16 bora baina ya Etoile du Sahel na Yanga unaotarajia kuanza leo majira ya saa 3:00 kwa saa za Tanzania.
Maelezo ya awali yataanza saa 2:00 usiku kupitia chaneli ya Azam TWO.
Azam TV kwa kuwajali watanzania wanaopenda soka imepambana kupata mechi hiyo licha ya kuwepo ugumu, lakini sasa imeshaipata rasmi baada ya Etoile du Sahel kufikia makubaliano na kituo hicho bora cha Matangazo ya mpira Afrika mashariki.
0 comments:
Post a Comment